Serikali kuwahusisha vijana katika ukuzaji wa Alizeti

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya kuimarisha uzalishaji wa alizeti.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo (KALRO), inalenga kuwaajiri wakulima vijana katika ukujazi wa alizeti, ili kuimarisha uzalishaji wa mafuta ya kupikia kwa lengo la kupunguza uagizaji mafuta hayo kutoka nje.

Mwenyekiti wa KALRO Dkt. Thuo Mathenge, alisema taasisi hiyo inalenga kuwahusisha takriban vijana 200 kutoka kila kaunti, katika ukuzaji wa alizeti, ikizingatiwa kuwa serikali iko tayari kutenga ekari 400 za ardhi kwa mpango huo.

“Tutawahusisha vijana kupitia vyama vya ushirika na kuwaunganisha na Hazina ya Vijana, Hazina ya Hustler na Shirika la Ufadhili wa Kilimo (AFC). Tunawataka wafahamu kuhusu kilimo, na kuwaelimisha kuhusu kilimo biashara,” alisema Dkt. Mathenge.

Kulingana na mwenyekiti huyo, serikali sasa ina ardhi, rasilimali na wanasayansi kuhakikisha ukuzaji wa alizeti unatekelezwa.

Alisema punde tu vijana watakapokuza mmea huo, serikali itanunu mitambo inayohitajika kuwawezesha vijana hao kupata mafuta na kusitisha hatua ya taifa hili kuagiza mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi.

“Tunaanza na alizeti, tunalenga kuzalisha mafuta ya kupikia hapa nchini, baadaye tutaingia katika uzalishaji wa mimea mingine.” aliongeza Dkt. Mathenge.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *