Olunga aondoka rasmi Al Duhail, baada ya miaka minne

Olunga alijiunga na Al Duhail, kwa kandarasi ya misimu mitatu akitokea Kashiwa Reysol ya Japan.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga, ameondoka katika klabu ya Al-Duhail Sports ya Qatar, baada ya kuwachezea kwa kipindi cha miaka minne.

Olunga alijiunga na Al Duhail, kwa kandarasi ya misimu mitatu, akitokea Kashiwa Reysol ya Japan.

Olunga, ambaye zamani alikuwa mshambulizi wa zamani wa klabu za Thika na Gor Mahia, anaondoka Al Duhail roho juu baada ya kupachika mabao 130, akiandikisha historia kuwa mfungaji bora wa timu hiyo.

Licha ya kugura Al Duhail,Olunga hajafichua timu atakayojiunga nayo.

Website |  + posts
Share This Article