Upasuaji wa Mwanablogu na Mwalimu Albert Omondi Ojwang, utafanyika leo kubaini chanzo cha kifo chake mikononi mwa polisi.
Usalama uliimarishwa nje na ndani ya makafani ya City mapema Jumanne,baada ya makundi ya wanaharakati wakiandamana na familia kuvuruga shughuli walipozingira eneo ambalo mwili huo umehifadhiwa Jumatatu .
Hatua hiyo ililazimu wapasuaji wa serikali kuahirisha shughuli hiyo hadi leo Jumanne.
Polisi walisema kuwa marehemu Ojwang alipatikana akiwa amepoteza fahamau katika kororkoro ya kituo cha Central, wakisema kuwa huenda lilikuwa jaribio la kujiua.
Ojwang pamoja na mshatikiwa mwingine Kelvin Moinde, walikabiliwa na kesi ya kuchapisha habari za uongo kumhusu Naibu Kamishnaa Mkuu wa Polisi Eliud Lagat.