Uchaguzi Mkuu Zambia: Hakainde Hichelema ashinda muhula wa pili

Mpinzani wake wa karibu, Brian Mundubile, amemaliza wa pili kwa kupata asilimia 38 ya kura zilizopigwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya Uchaguzi nchini Zambia mapema leo Jumanne imemtangaza Rais Hakainde Hichilema kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Alhamisi wiki jana baada ya kuzoa asilimia 60 ya kura.

Mpinzani wake wa karibu, Brian Mundubile, amemaliza wa pili kwa kupata asilimia 38 ya kura zilizopigwa.

Hii ni kulingana na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa tume hiyo, Mwangala Zaloumis.

Matokeo hayo yametangazwa licha ya kusalia na maeneo bunge matano ambayo zoezi la ujumuishaji kura halijakamilika.

Yamkini hatua hiyo ni kutokana na ukweli kwamba matokeo hayo huenda yasibadilishe matokeo ya mwisho.

Share This Article