Vyama vya Walimu nchini vimekuja kwa matao ya juu kupinga masharti mapya yaliyotolewa na Tume ya Kuwaajiri ya TSC, iliyotaka walimu wote wadhibitiwe kutumia mitandao ya kijamii.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya walimu wameitaka TSC itoe ufafanuzi zaidi kuhusu masharti hayo.
Wameikosoa hatua hiyo wakisema inalenga kukiuka haki zao za kikatiba na kuwakandamiza.
Chama cha Walimu cha KNUT kilitaja hatua hiyo kuwa inayolenga kuwanyamazisha walimu ambao wamekuwa wakipaza sauti sana mitandaoni kikiitaja kuwa ni ya kuwanyima walimu uhuru wa kujieleza.
Wiki jana, TSC ilitishia kuwaadhibu walimu wanaojihusisha katika unyanyasaji mitandaoni na wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya.