Mama Taifa ahimiza elimu kati ya jamii za wafugaji

Alisema kuwa ni kupitia elimu pekee ndipo wataweza kuvunja minyororo ya ukosefu wa maendeleo na kukumbatia usasa

Marion Bosire
1 Min Read
Mama Taifa Rachel Ruto.

Mkewe Rais, Rachal Ruto, amewahimiza jamii za wafugaji katika eneo la Laikipia Kaskazini kukumbatia elimu kama mkakati wa kuondoa umaskini.

Mama taifa alisema kuwa ni kupitia elimu pekee ndipo wataweza kuvunja minyororo ya ukosefu wa maendeleo na kukumbatia usasa.

Alikuwa akizungumza katika Wadi ya Segera, kaunti ya Laikipia, wakati wa kuzindua rasmi madarasa ya Shule ya Msingi ya Segera Mission Junior.

Mama Rachel aliwahimiza wafugaji kwenda sambamba na mabadiliko ya maisha ya sasa na kuifanya elimu kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Alijitolea kuunga mkono azma ya Rais ya kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa wote.

Viongozi wa eneo hilo wamepongeza hatua hiyo, huku wakiisifu serikali kwa kurejesha usalama katika eneo lenye changamoto la Laikipia Kaskazini.

Hatua hiyo imewezesha kurejeshwa kikamilifu kwa huduma za elimu katika maeneo yaliyokuwa yameathiriwa hapo awali.

Share This Article