Serikali yafafanua amri ya kuwatimua raia wa kigeni wasio na vibali nchini Kenya

Pia serikali imewaonya maafisa wa Polisi dhidi ya kutumika kuwahangaisha raia wa kigeni walio humu nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu amri iliyotolewa na Rais William Ruto wiki jana ya kufanywa kwa msako kwa raia wote wa kigeni wasio na vikabali wanaofanya biashara humu nchini.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa serikali Charles Owino imewataka raia wote wa kigeni wanaoishi nchini Kenya kufika kwa balozi zao ili kusajiliwa kisha baadaye taarifa hiyo ikabidhiwe serikali ya Kenya.

Hatu hiyo inalenga kuwalinda raia wa kigeni walio humu nchini na pia maslahi ya Wakenya.

Hata hivyo, serikali imetoa tahadhari dhidi ya visa vyovyote vya wakenya kuwadhulumu raia hao kigenini hususan wale kutoka Burundi.

Pia serikali imewaonya maafisa wa polisi dhidi ya kutumika kuwahangaisha raia wa kigeni walio humu nchini.

Msemaji wa serikali amesema punde usajili wa raia wote wa kigeni utakapokamilika serikali ya Kenya itafanya utathimini wake .

Pia serikali imevionya vyombo vya habari dhidi ya kupotosha umma na kuzua taharuki kupitia kwa kutoa ripoti za kupotosha kuhusu amri hiyo.

Share This Article