Wanariadha 14 wa Kenya ni miongoni mwa wanariadha 381 kutoka mataifa 65, wanaotarajiwa kushiriki makala ya kwanza ya mashindano ya Ultimate, yatakayoandaliwa mjini Budapest,Hungary baina ya Septemba 11 na 13 mwaka huu.
Bingwa wa Dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot, atatimka mita 1,500 pamoja na Phanuel Kosgei.
Mbio za mita 5,000 zitashuhudia Jaco Krop na Cornelius Kemboi wakishiriki,wakati bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi akitimka mita 800 naye bingwa wa Afrika Julius Yego, atashiriki urushaji sagai.
Aidha,Mercy Oketch, atakimbia mita 400 huku pia kijumuishwa katika timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti mseto.

Phanuel Kosgei akishiriki mita 1,500 mashindano ya Brussels Diamond League
Kenya itawakilishwa na timu ya mita 400 inayowajumuisha George Mutinda,Boniface Mweresa,Kelvin Kiprotich na Lanoline Aoko.
Mashindano hayo ambayo yatakuwa na donge nono la pesa la kima cha shilingi bilioni 1.3, huku mabingwa wa kila mabingwa wa kila fani wakituzwa shilingi milioni 19.4
Mashindano hayo yanawashirikisha mabingwa wa Olimpiki,Mabingwa wa Dunia na mabingwa wa Diamond League katika fani 28 tofauti.