KURA kufunga barabara kadhaa Nairobi kwa shughuli za ujenzi

Barabara hizo ni pamoja na sehemu ya barabara ya Ngong, Kenyatta Avenue, Valley Road na ile ya Jakaya Kikwete.

Tom Mathinji
1 Min Read
Baadhi ya barabara Nairobi kufungwa, kutoa fursa kwa shughuli za ujenzi.

Mamlaka ya Barabara za Miji nchini (KURA) imetangaza kufungwa kwa baadhi ya barabara jijini Nairobi ili kutoa fursa kwa shughuli za ujenzi.

Kwenye ilani kwa umma, KURA ilisema barabara hizo ambazo ni pamoja na sehemu ya barabara ya Ngong, Kenyatta Avenue, Valley Road na ile ya Jakaya Kikwete, zitafungwa kwa muda wa miezi minane kati ya Ijumaa Juni 12, 2026 hadi Ijumaa, Februari 12, 2027.

“Hatua ni kutoa fursa kwa mwanakandarasi kutekeleza ujenzi wa daraja, huku akihakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara. Tunawahimiza madereva kutumia barabara mbadala,” ilisema ilani hiyo ya KURA.

Aidha, mamlaka hiyo ilisema sehemu ya barabara ya Ngongo kati ya Windy Ridge  na Westwood Park huko Karen itafungwa kwa muda wa juma moja kuanzia Juni 11, 2026 kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa mitaro ya kuelekeza maji.

Wakati huo huo, sehemu za barabara ya Haile Selassie zitafungwa kwa muda wa wiki nne kutoa fursa ya ujenzi wa daraja.

TAGGED:
Share This Article