Serikali yatoa wito wa usalama thabiti wa mtandaoni

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Raymond Omollo - Katibu wa Usalama wa Taifa

Serikali imeelezea dhamira yake ya kuimarisha mfumo wa usalama wa mtandaoni nchini na kuendeleza mipangokazi thabiti ya udhibiti wa teknolojia zinazoibuka, ikiwa ni pamoja akili unde, AI. 

Katibu wa Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo amesema lengo ni kulinda uchumi wa kidijitali unaopanuka kwa kasi nchini.

“Mabadiliko ya kidijitali yameibuka kuwa siyo tu kichocheo muhimu cha ukuaji uchumi, utoaji huduma ya umma na uwazi serikalini, bali pia yameongeza hatari za matishio ya mitandaoni yanayohitaji hatua za kitaifa zilizoratibiwa,” alisema Dkt. Omollo.

Aliyasema hayo wakati akifungua Mkutnao wa Sita wa kila Mwaka wa Mifumo ya Usimamizi wa Usalama wa Taarifa (ISMS) mjini Naivasha.

Dkt. Omollo alisema ajenda ya mabadiliko ya kidijitali ya serikali chini ya Ajenda ya Kutoka Juu had Chini (BETA) inaendelea kuongeza kasi ya utoaji huduma za umma kupitia majukwaa ya kidijitali nchini.

Alitoa mfano wa mfumo wa eCitizen aliyosema kwa sasa unatoa huduma zaidi ya 24,000 za serikali kwa umma na kutumiwa na watumiaji zaidi ya milioni 15.

 

 

Share This Article