Xavier Nato ambaye ni mwandishi wa hati za maigizo anahitaji usaidizi wa kifedha kugharamia matibabu.
Kulingana na bango linalosambazwa mitandaoni, Nato ambaye pia ni mwigizaji aliugua kiharusi ambacho kilimsababishia matatizo ya figo.
Mmiliki huyo wa kampuni ya uigizaji ya Millaz Productions amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na anahitaji matibabu spesheli ambayo ni ghali.
Mwigizaji mwenza Kenneth Ambani alichapisha bango hilo kwenye akaunti yake ya Facebook ambapo alisema kwamba wasanii wengi hutegemea tu usanii wao kujikimu kifedha.
“Xavier Nato ni mmoja wa wasanii hao wengi. Ndugu anahitaji usaidizi wetu ili tumrejeshe kwa familia yake, kazi yake na sanaa.” aliandika Ambani.
Ambani ambaye ni mwanachama wa kamati kuu ya serikali ya kaunti ya Mombasa anayesimamia masuala ya vijana, jinsia, michezo na jamii amehimiza wakenya kumchangia Xavier.
Ili kumchangia Xavier Nato, unaweza kutuma pesa kwa nambari ya ya Paybill 891300 nambari ya akaunti ikiwa 107088.
Kampuni ya Xavier ya Millaz Productions kuandaa na kuonyesha maigizo ya jukwaani kwenye ukumbi wa Kenya National Theatre.