Mshukiwa mkuu katika kesi ya Kim Kardashian afariki

Kim Kardashian alivamiwa na wakora walioiba mali yake jijini Paris nchini Ufaransa mwaka 2026 kesi inayotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Marion Bosire
2 Min Read

Mmoja wa washukiwa wakuu katika kisa ambapo mwamitindo Kim Kardashian aliibiwa jijini Paris nchini Ufaransa ameripotiwa kufariki ghafla, muda mfupi kabla ya kuanza kwa kesi dhidi yake.

Kulingana na Daily Mail, Marceau Baum-Gertner alifariki Machi 6 jijini Paris na kilichosababisha kifo chake bado hakijabainishwa.

Marceau alilaumiwa kwa kushirikiana na genge fulani ambalo lilimvamia Kim Kardashian mwaka 2016 na kumzuilia kwa muda wakimtishia kwa bunduki.

Kesi dhidi ya jamaa huyo wa umri wa miaka 72 ilitarajiwa kuanza leo ambapo wanakabiliwa na mashtaka kadhaa kama vile kumwibia Kim dola milioni 10.

Kim Kardashian naye anatarajiwa kutoa ushahidi mahakamani katika kesi hiyo jijini Paris mwezi mei mwaka huu wa 2025.

Awali mfanyabiashara huyo alikuwa amemwelezea jaji kuhusu kisa hicho cha wizi kilichomkumba lakini sasa atapata fursa ya kuhadithia kwa kina matukio ya usiku huo.

Marehemu Baum-Gertner alikuwa amekataa kutaja wahusika wengine kwenye kisa hicho cha wizi wa kimabavu wakati alihojiwa kabla ya kesi kuanza rasmi.

Kulingana na ripoti ya kabla ya kesi hiyo kuanza, kulikuwa na uwezekano wake kuwataja kama njia ya kupunguziwa adhabu dhidi yake.

Oktoba 3, 2026,saa nane unusu alfajiri, akiwa kwenye chumba chake cha malazi, Kim Kardashian alivamiwa na wanaume watatu waliokuwa wamefunika nyuso zao na walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Alikuwa amebakia peke yake ya ajili ya mapumziko huku aliokuwa nao wakiwemo dadake na mlinzi wake wakikwenda kujivinjari jijini Paris.

Watu hao walimtishia, wakamfunga mdomo, mikono na miguu kisha wakamtaka awape pete yake ambayo ilikuwa ghali pamoja na pesa.

Waliondoka na bidhaa mbali mbali zinazokisiwa kuwa za thamani ya dola milioni 10, ikiwemo pete yake ya uchumba aliyokuwa amevishwa na Kanye West ya thamani ya dola milioni 4.

Website |  + posts
Share This Article