Mamake Beyonce apongeza Grammys kwa kutambua wasanii weusi

Wasanii ambao ni wamarekani weusi kama vile binti yake Beyonce, Kendrick Lamar, Doechii na wengine waling'aa kwenye awamu ya 67 ya tuzo za Grammy.

Marion Bosire
2 Min Read

Tina Knowles mama mzazi wa msanii wa muziki Beyonce amepongeza tuzo za Grammy kwa kutambua wasanii weusi “nyakati hizi za ubaguzi wa rangi”.

Hii ni baada ya binti yake kushinda tuzo kadhaa za Grammy ikiwemo ya kitengo cha Albamu bora ya mtindo wa Country kwa albamu yake iitwayo “Cowboy Carter”.

“Inabidi nipongeze waandalizi wa tuzo za Grammy kwani katika nyakati mbaya zaidi za ubaguzi wa rangi, huku kila mmoja akihisi shinikizo za kupuuza mafanikio ya watu weusi, wamechukua hatua na kufanya yanayfaa.” aliandika mama huyo kwenye mitandao ya kijamii.

Wasanii ambao ni wamarekani weusi kama vile binti yake Beyonce, Kendrick Lamar, Doechii na wengine waling’aa kwenye awamu ya 67 ya tuzo za Grammy.

Tina alifafanua kwamba katika miaka iliyopita aliamua kutohudhuria hafla za kutoa tuzo za Grammy kwa sababu ya kile anachokitaja kuwa ukosefu wa usawa hasa kwa wasanii weusi.

Kulingana naye wasanii hao wamekuwa wakitumiwa kurembesha hafla za tuzo hizo na kisha kupatiwa tuzo za kuwapoza moyo tu lakini mwaka huu imekuwa tofauti.

Alimpongeza mkurugenzi mkuu wa akademia andalizi ya tuzo za Grammy Harvey Jay Mason Jr. kwa kushughulikia mabadiliko kadhaa baada ya tuzo za Grammy kukosolewa na wengi kwa kile kilichotajwa kuwa kukosa ujumuishaji.

“Niliguswa na hotuba ya Harvey Mason na kujitolea kwake kwa mabadiliko. Kwa hivyo asante Grammys kwa ujasiri wa kufanya jambo linalostahili.” aliongeza kusema Tina Knowles.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *