Kongamano la Ugatuzi la mwaka 2025 litaandaliwa katika kaunti ya Homa Bay kati ya Agosti 12-15, 2025.
Hii imetangazwa leo Jumanne baada ya kukamilika kwa mkutano wa kamati inayoratibu kongamano hilo mwaka huu.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Magavana Gladys Wanga wa Homa Bay na Mutahi Kahiga wa Nyeri miongoni mwa viongozi wengine.
Kongamano la Ugatuzi hutumiwa kupigia msasa hatua iliyopigwa katika utekelezaji wa ugatuzi tangu kuasisiwa kwake.
Mawaziri, Magavana, Maseneta, wabunge na wataalam katika nyanja mbalimbali ni miongoni mwa viongozi ambao kwa kawaida uhudhuria kongamano hilo.