Msanii wa mtindo wa Afrobeat kutoka Nigeria Tems hatimaye amemtambua Seyi Sodimu, ambaye ana jukumu kubwa katika uandishi wa wimbo uliomshindia tuzo ya Grammy “Love Me Jeje”.
Tems ambaye jina lake halisi ni Temilade Openiyi alikosolewa na wengi mitandaoni kwa kukosa kumtaja Seyi wakati wa hotuba ya kukubali tuzo hiyo.
Tems anaripotiwa kutoa maneno mengi ya wimbo huo kwa wimbo wa Seyi wa mwaka 1997 na kupitia mitandao ya kijamii hususan X, Tems ametoa shukrani kwa Seyi kwa kumkubalia kutumia wimbo huo wake.
Alichapisha picha akiwa na Seyi na kuansika, “Nataka tu kumshukuru Seyi kwa jukumu lake katika kusaidia kupata idhini ya kutumia wimbo wake ‘Love me Jeje'”.
Mwanamuziki huyo aliendelea kusema kwamba wimbo wake ulihuisha wimbo wa awali wa Seyii na anafurahia kwamba sasa anapata pongezi anazostahili.
“Wimbo bora wa nyakati zote. Ninakushukuru sana. Asante kwa mapenzi yako na usaidizi.” alimalizia Tems.
Seyi kwa upande wake amekubali shukrani za Tems ambaye amemrejelea kuwa ‘Princess’ akisema anastahili usaidizi kama huo na kwamba mazuri yako mbele.