Ufaransa imetangaza kuinga mkono Morocco katika mzozo wa Sahara uliodumu miongo kadhaa baina ya Morocco na Algeria.
Haya yametangazwa mapema wiki hii na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipohutubia mabunge mawili ya Morocco kwenye ziara yake nchini humo.
Macron aliahidi kuwa serikali yake itawekeza katika eneo la Sahara na pia Morocco.
Western Sahara ni eneo lililo kaskazini mwa pwani ya Afrika, ambalo limekuwa likizozaniwa kwa miongo kadhaa kati ya Morocco na Algeria.
Sahara ilitawaliwa na Wahispania ila kwa sasa inamilikiwa na Morocco kwa kiwango kikubwa huku pia sehemu ndogo ikiwa chini ya wanamgambo wa Algeria.
Algeria imekuwa ikikashifu vikali uwepo wa Morocco katika eneo hilo wakilitaka liwe nchi huru.
Tamko la Macron mapema Julai mwaka huu la kuunga mkono Morocco katika mzozo huo liliikasirisha Algeria iliyofunga ubalozi wake nchini Ufaransa.