Kindiki kuapishwa au kutoapishwa kubainika leo mahakamani

Dismas Otuke
1 Min Read
Prof. Kithure Kindiki, kuapishwa kuwa Naibu Rais Ijumaa.

Kitendawili cha endapo Naibu Rais mteule Profesa Abraham Kithure Kindiki ataapishwa rasmi kumrithi Rigathi Gachagua kitateguliwa leo Alhamisi.

Hii ni pale jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu litakapotoa uamuzi wake kuhusu maagizo yaliyozuia uapisho huo.

Majaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Dkt. Fred Mugambi wanatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu na Bunge ya kutaka kuondolewa kwa maagizo hayo.

Gachagua kupitia kwa mawakili wake alipata maagizo ya kuzuia kuapishwa kwa Prof. Kindiki punde baada ya kuteuliwa kwake.

Anataka maagizo hayo kutoondolewa hadi pale kesi ya kupinga kutimuliwa kwake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Bunge la Taifa lilikuwa la kwanza kupiga kura ya kumtimua Gachagua, uamuzi ambao uliungwa mkono na Bunge la Seneti.

Website |  + posts
Share This Article