Rais Ruto amwomboleza Aga Khan

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto amemwomboleza kiongozi wa kidini wa kundi la Kiislamu la Ismaili, Aga Khan, aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 88.

Rais Ruto alimtaja Aga Khan kuwa kiongozi aliyejizatiti kwa udi na uvumba kuboresha maisha ya watu katika jamii.

“Tumehuzunishwa na kifo cha Aga Khan, kiongozi wa kidini wa kundi la Kiislamu la Ismaili. Alikuwa kiongozi aliyetia bidii kuwasaidia watu kupitia shughuli zake za utoaji misaada katika shule na hospitali. Mawazo yetu yako pamoja na familia yake na pamoja na jamii ya Kiislamu ya Ismailia,” alisema Rais Ruto.

Sultan Aga Khan, mwanzilishi na mwenyekiti wa kituo cha maendeleo cha Aga Khan (AKDN), aliongoza shughuli nyingi za utoaji misaada ambazo zilijumuisha shule, hospitali na miradi ya kitamaduni hususan katika mataifa yanayostawi

Nchini Kenya, AKDN  iliongoza biashara kama vile kampuni ya  Nation Media Group, Chuo Kikuu cha Aga Khan, hospitali na shule za Aga Khan.

Zingine ni pamoja na benki ya Diamond Trust Bank (DTB), kampuni ya bima ya Jubilee na kampuni ya Farmers Choice.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *