Police, Gor Mahia washinda Tusker wakabana koo na Shabana Ligi Kuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya, Police FC, wamesajili ushindi wa kwanza msimu huu baada ya kuwalemea wenye APS Bomet FC waliopandishwa ngazi msimu huu.

Mechi hiyo imesakatwa katika uwanja wa Kericho Green, bao pekee la Police likipachikwa na Clinton Kilanga mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kudumu hadi kipenga cha mwisho.

Police wana alama nne baada ya kuambualia sare tasa na Ulinzi Stars wiki jana katika pambano la ufunguzi.

Katika mechi nyingine, Gor Mahia wameishinda KCB bao moja kwa bila, huku Tusker FC wakitoka nyuma na kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Shabana FC uwanjani Kasarani.

Kariobangi Sharks iliwalemea Matahre United mabao 2-1, wakati Mara Sugar ikiwakosea adabu Ulinzi Stars kwa kuwaadhibu goli moja bila jibu.

Shabana wanaongoza jedwali kwa pointi 7 sawa na Posta Rangers, alama moja mbele ya Gor na KCB walio katika nafasi za 3 na 4 mtawalia.

Website |  + posts
Share This Article