Bingwa wa dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 Edmund Serem, amemaliza wa pili katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji katika mkondo wa pili ulioandaliwa leo mjini Shanghai,China.
Serem ametumia dakika 8 sekunde 8.46 nyuma ya Abrhm Sime wa Ethioipia, aliyezitimka kwa dakika 8 sekunde 7.2 huku Mkenya mwingine Simon Koech, akiridhia nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 8 sekunde 9.05.
Nicholas Kipkorir, alimaliza wa nne kwenye fainali ya mita 5,000, kwa dakika 12 sekunde 56.81.
Berihu Aregawi, amewaongoza Waethiopia, kutwaa nafasi tatu bora akitumia muda wa dakika 12 sekunde 50.45.
Bingwa wa Jumuia ya Madola katika mita 100, Ferdinand Omanyala, amevuta mkia kwa sekunde 10.25.
Akani Simbine, kutoka Afrika Kusini, amesajili ushindi baada ya kutimka kwa sekunde 9.98,mbele ya mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki Kishane Thompson, wa Jamaica, amemaliza wa pili kwa sekunde 9.99, huku bingwa wa Olimpiki katika 200 kwa sekunde 10.03.