Shirika la ndege nchini Rwanda, RwandaAir, limetangaza kurejelea tena safari zake za Kigali, Zanzibar na Mombasa likiwalenga watalii wanaozuru fukwe za miji hiyo.
RwandaAir itatumia ndege aina ya Boeing 737 ambayo itakuwa ikisafiri mara nne kwa kila wiki katika maeneo hayo matatu.
Shirika la Ndege la Kenya Airways tayari lina safari 13 kwa kila wiki kuunganisha miji hiyo ya pwani ya Afrika mashariki huku ujio wa RwandaAir ukitarajiwa kutoa ushindani mkali kwani pia Jambo Jet husafirisha abiria kati ya Mombasa na Zanzibar.