Mshikilizi wa Rekodi ya Dunia ya kilomita kumi Agnes Jebet Ng’etich ameshinda makala ya mwaka huu ya mbio za Valencia Half Marathon zilizondaliwa Jumapili nchini Uhispania.
Ng’eticha ameweka muda wa kasi duniani wa lisaa 1 dakika 3 na sekunde 8 kutwaa ubingwa na kuhifadhi taji yake huku akikosa sekunde 16 pekee avunje rekodi ya Dunia.
Fotyen Tesfay kutoka Ethiopia amemaliza wa pili kwa lisaa 1 dakika 5 na sekunde 11, sekunde 35 mbele ya Mkenya Veronicah Lelo aliyechukua nafasi ya tatu.
Yomif Kejelcha wa Ethiopia pia alihifadhi taji ya wanaume kwa dakika 58 na sekunde 2 huku Brian Kibor wa Kenya akiridhia nafasi ya tatu.