Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula ametetea sheria mpya zilizopitishwa na Wabunge na kuidhinishwa na Rais William Ruto, akisema zinalenga kuleta ustaarabu mitandaoni , kuzuia itakadi kali na uchochezi mitandaoni.
Wetang’ula amesema haya siku ya Jumapili alipohudhuria ibada katika kanisa la Katoliki la St. Teresa’s Isanjiro mjini Malava kaunti ya Kakamega .
Akikariri manufaa makubwa yaliyoletwa na utandawazi wa mitandao kama vile biashara,mawasiliano na elimu serikali inalenga kuzuia matumizi mabovu kama vile sinema za ngono kwa watoto na uhalifu wa mitandaoni .
Wetang’ula aliandamana na kiongozi wa wengi Bungeni Kimani Ichung’wah, aliyekanusha madai kuwa serikali inalenga kubana uhuru wa kujieleza nchini.