KWS yafungua tena uwanja wa ndege wa Amboseli

Dismas Otuke
1 Min Read

Huduma ya kitaifa ya Wanyamapori (KWS), imetangaza kufungua tena uwanja mdogo wa ndege wa Amboseli, takriban miezi miwili baada ya kuufunga .

Uwanja wa Amboseli ulifungwa baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa.

Uwanja huo umefunguliwa kufuatia uchunguzi uliofanywa na KWS Mei 7.

KWS ilitangaza kufunga uwanja huo tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu baada ya mvua kubwa kusabisha mafuriko.

Mamlaka ya usafiri wa angani (KCAA) imeondoa marufuku iliyokuwa imeweka kwa matumizi ya uwanja huo kwa ndege za watalii.

Ndege badala yake zimekuwa zikitumia uwanja ulio karibu wa Tawi kilomita 5 kutoka Kimana.

Share This Article