Klabu ya USM Alger kutoka Algeria iwaalika Zamalek kutoka Misri, kwenye duru ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mechi hiyo itang’oa nanga saa nne usiku huku marudio yakiandaliwa wiki ijayo nchini Misri ambapo mshindi wa jumla atatuzwa dola milioni 4 za Marekani.
USMA wanawinda kombe hilo kwa mara ya pili baada ya kutwaa ubingwa mwaka 2023, walipowashinda Yanga wakati Zaamalek, wakiwinda taji ya tatu baada ya kuibuka kidedea mwaka 2019 na mwaka 2024.

Itakuwa mara ya tatu kwa miamba hao wawili kumenyana baada ya kutoka sare katika mkondo wa kwanza nao USMA wakashinda duru ya pili mwaka 2017.