Mariga asema hakuna pengo la uongozi FKF baada ya kufurushwa kwa Rais Mohammed

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF McDonald Mariga, amekanusha kuwepo kwa pengo la uongozi kufutia hatua ya baraza kuu NEC kumtimua  Rais Hussein Mohammed siku ya Ijumaa.

Akiwahutubia Wanahabari Jumamosi adhuhuri, Mariga amewataka wafadhili kuwekeza na kushirikiana na FKF .

Akiandamana na wanachama wengine saba wa  kamati kuu ,Mariga amesema shirikisho liko imara akiwataka wadhamini zaidi kujiunga na FKF.

Wanachama wanane kati ya  tisa waliopiga kura ya kumtimua Hussein walihudhuria kikao hicho cha wanahabari.

Mariga ameahidi kuitisha mkutano wa dhaharura wa kamati  kuu, ili kuratibu mambo kadhaa ikiwemo kufanya ukaguzi wa mikataba yote iliyopo.

Pia Mariga ametetea hatua ya wanachama wa kamati kuu kuwatimua afisini Hussein pamoja na Katibu Mkuu ili kupisha uchunguzi.

 

Share This Article