Shirkisho la kandanda ulimwenguni -FIFA, litaandaa sherehe tatu tofauti za kufungua makala ya 23 ya kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia katika mataifa ya Marekani,Mexico na Canada.
Mexico itaandaa sherehe za ufunguzi Juni 11 ikifuatwa na Marekani, na Canada, watakaofanya sherehe za ufunguzi Juni 12.
Mexico watacheza na Afrika Kusini katika mechi ya ufunguzi Juni 11,ikifuatwa na Canada dhidi Bosnia Herzegovina na Marekani dhidi ya Paraguay Juni 12.
Jumla ya mechi 104 zitachezwa katika miji 16 tofauti huku fainali ikisakatwa Julai 19, uwanjani New York New Jersey.