Timu nne zarejea kucheza robo fainali Kombe la Dunia mwaka huu

Argentina waliotwaa kombe hilo mwaka 2022,watahitimisha robo fainali dhidi ya Uswizi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu nne kati ya nane zilizocheza hadi robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022,zitarejea kucheza ktika kwota fainali ya mwaka huu huku kipute hicho kikirejea leo kwa kwota fainali.

Ufaransa walioshindwa katika fainali ya mwaka 2022 na Argentina, watafungua mechi za nane bora Alhamisi, usiku dhidi ya Morocco, ambao walimaliza katika nafasi ya nne.

Uingereza ambayo pia ilikuwa katika robo fainali ya makala yaliyopita, pia imefuzu mwaka huu ikipangiwa kuchuana na Norway, ambao watakuwa robo fainali kwa mara ya kwanza.

Robo fainali nyingine ya mwaka huu itawashirikisha Uhispania na Ubelgiji ambao wote walikosa kufika robo fainali .

Argentina waliotwaa kombe hilo mwaka 2022,watahitimisha robo fainali dhidi ya Uswizi.

Share This Article