Serikali ya Msumbiji yatoa ruzuku kwa sekta ya uchukuzi kuzuia nauli kupanda

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Msumbiji kupitia kwa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, imeanza kutekeleza utoaji wa ruzuku kwa wamiliki wa magari ya usafiri wa umma, ili kuzuia kupanda kwa nauli kufuatia kuongeza kwa bei ya mafuta.

Kwa mujibu wa  arifa ya serikali hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mazungumzo ya kina baina ya pande mbili kama njia ya haraka ya kuwapunguzia raia mzigo wa ongezeko la bei ya mafuta.

Kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na vita vya Israel na Marekani, nchini Iran, kumesababisha ukosefu au upungufu wa mafuta hali ambayo imesababisha kupaa kwa bei ya bidhaa za petroli na mafuta.

Serikali na shirikisho la vyama vya uchukuzi wa barabarani (FEMATRO), zimewataka wenye magari kutopandisha bei za nauli kwa abiria, wakisisitiza kuwa watawafidia kwa gharama ya juu ya mafuta.

Lita moja ya Petroli nchini Msumbiji, imepanda hadi shilingi 186 za Kenya, kutoka kwa bei ya awali ya shilingi 160 za Kenya, huku bei Dizeli ikipanda kutoka shilingi 161 hadi shilingi 234 za kenya.

Share This Article