Seneta wa Nakuru Tabitha Karanja ametangaza kugura chama tawala cha United Democratic Alliance, UDA na kujiunga rasmi na kile cha Democracy for the Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Karanja amekaribishwa rasmi katika chama cha DCP na Gachagua, siku moja tu baada ya mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba kuhama UDA na kujiunga na DCP.
Karanja alitangaza hayo Ijumaa katika kikao cha kisiasa kaunti ya Nakuru ambapo pia alitangaza azma ya kuwania Ugavana wa kaunti hiyo.
Karanja alijiunga na UDA mwezi Januari mwaka 2022 na kuchaguliwa kuwa Seneta.