Waziri mwenye Mamlaka Makuu wa Kenya Musalia Mudavadi, amehimiza haja ya mazungumzo baina ya pande zote zinazohusika katika mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa suluhu pekee na wala sio vita.
Akihutubu leo katika siku ya kwanza ya kongamano lisilo la kawaida linalojumuisha Jumuia ya Afrika Mashariki—EAC, na Jumuia ya Manendelo Kusini mwa Afrika-SADC, jijini Dar es Salaam, Mudavadi amesema ipo haja ya pande zote kusitisha mapigano ili kupisha mazungumzo.
Mudavadi pia ameelezea msimamo wa Kenya akisema wanahimiza pande zote kuwa mezani katika mazungumzo ya kuleta amani nchini DRC.
Mudavadi aliongoza kikao hicho cha mawaziri ambacho kilitangulia kongamano la kesho la Marais.