Mwenyekiti wa KBC amwomboleza mtangazaji nguli Mambo Mbotela

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika shirika la utangazaji nchini KBC.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Shirika la Utangazaji hapa Nchini (KBC) Tom Mshindi, ametuma risala za rambirambi kwa familia na marafiki wa mtangazaji mkongwe Leonard Mambo Mbotela, aliyefariki siku ya Ijumaa.

Katika risala hizo, Mshindi alimtaja Mbotela sio tu mwenye sauti iliyowavutia wengi, lakini pia aliyewakuta wengi katika tasnia ya utangazaji.

“Kipindi cha, Je, Huu Ni Ungwana?, kilileta mwangaza katika jamii na pia kilisaidia kukuza maadili na heshima katika jamii,” alisema Mshindi.

“Kama Shirika la KBC, tunamuenzi kwa kushikilia maadili aliyopigia debe , utaalam na huduma kwa taifa,” aliongeza Mshindi.

Mwanaye, Jimmy Mbotela, aliithibitishia KBC kwamba Leonard Mambo Mbotela alifariki Ijumaa saa tatu na nusu akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi South. Mambo alifariki akiwa na umri wa miaka 85.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *