Wizara ya Afya yawaajiri Wahudumu wa Afya wanagenzi 6,484

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Afya Aden Duale.

Wizara ya afya imeajiri rasmi kundi la kwanza la wahudumu wa afya wanagenzi wapatao 6,484 kwa kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2025/2026.

Kulingana na waziri kwa afya Aden Duale wahudumu hao wataanza kazi tarehe mosi mwezi Julai, kwenye kile alichotaja kama hatua muhimu iliyoashiria kujitolea kwa serikali kulainisha na kuboresha idadi ya wahudumu wa afya waliohitimu nchini.

Alisema wahudumu hao watapelekwa katika hospitali mbalimbali nchini ambako watahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja chini ya mpango wa kimasomo kwa wahudumu hao.

Wahudumu hao ni pamoja na madaktari wa kawaida wapatao 1,147, madaktari wanagenzi wa meno 87, wahudumu wa utoaji dawa 500, maafisa wa kliniki 659 walio na shahada ya digrii, maafisa wa kliniki 1,993 waliona diploma na wauguzi  2,098 waliohitimu na shahada ya digrii.

Wizara imewaagiza wahudumu hao kuchukua barua zao katika makao makuu ya wizara ifikiapo jumatatu tarehe 30 mwezi huu wa juni.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article