Marekani yasimamisha ufadhili wa operesheni ya usalama nchini Haiti

Tom Mathinji and BBC
2 Min Read
Maafisa wa polisi washika doria nchini Haiti.

Ufadhili wa dola zaidi ya milioni 13 unaotolewa na Marekani kwa operesheni ya vikosi vya usalama vya kimataifa vinavyopambana na magenge ya Haiti umesitishwa kwa muda wa siku 90, umesema Umoja wa Mataifa (UN).

Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuagiza misaada ya nje ya Marekani isitishwe na ihakikiwe ili isukwe kulingana na maslahi ya taifa hilo.

Magenge hatari yaliyo na silaha zinazodaiwa zimetoka Marekani yapo katika mji mku wa Port-au- Prince yakidhibiti mji na kuvamia maeneo tofauti nchini Haiti.

Misheni ya usalama ya kimataifa iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC, sio operesheni ya UN bali inategemea misaada kutoka mataifa yaliyoendelea.

Misheni hiyo kufikia sasa haijafanya cha mno kuhakikisha hali ya usalama imerejea katika taifa la Haiti ambalo limekuwa likihangaishwa na magenge hayo.

Kuna zaidi ya maafisa wa polisi 900 kutoka Kenya, vikosi vya El Salvador, Jamaica, Guatemala na Belize.

Dola za Kimarekani zaidi ya milioni 110 zimewekezwa katika mfuko wa misheni ya UN, kiasi kikubwa kikitoka Canada, kulingana na data za UN.

“Marekani iliahidi kutoa dola milioni 15 kwa mfuko huo wa kufadhili operesheni hiyo, dola milioni 1.7 zilikuwa tayari zimetolewa, zikisalia dola milioni 13.3 ambazo zimesitishwa,’’ msemaji wa UN Stephane Dujarric amewaambia wanahabari.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *