Hofu imezuka katika kanti ya Kisii, kufuatia kuzuka kwa ugonjwa mpya usiojulikana katika siku za hivi maajuzi.
Kulingana na Katibu wa Afya ya umma Mary Muthoni, visa 11 vipya vimeripotiwa na kufikisha jumla ya idadi ya visa 168 vilivyonakiliwa.
Ugonjwa huo umeripotiwa katika vijiji vinane huku kitongoji cha Amarondo, kikiwa na asilimia 64 ya wagonjwa na inakisiwa kuwa unasababishwa na maji machafu.
Aidha, Muthoni amesema wanashirikiana na serikali ya kaunti ya Kisii kuthibiti ugonjwa huo na kuzuia kuenea,baada ya kupatikana kwa visa vipya.
Baadhi ya mbinu za kuzuia ugonjwa huo zilizowekwa na serikali ni pamoja na; usambazaji wa dawa za kutakasa maji na kuzingatia usafi, wakati pia mipango ikiwekwa ya kuanza kutoa dawa za minyoo kwa wanafunzi na kutakasa maji ya kunywa.
Muthoni aliongeza pia kufikia sasa wizara yake imesambaza tembe 44,350 kwa wakazi wa vijiji vilivyo na wagonjwa.
Wagonjwa walioathiriwa wamekuwa na dalili kama vile kuumwa na viungo vya mwili, kuumwa na kichwa, kuendesha, na kuyeyuka kwa tumbo.