Kenya yajiandaa dhidi ya Gambia na Gabon kufuzu Kombe la Dunia

Harambee Stars inashikilia nafasi ya nne kundini kwa alama tano baada ya mechi nne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, imeripoti kwa kambi ya mazoezi jana katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, kujiandaa kwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Gambia na Gabon.

Kocha Benni McCarthy aliongoza mazoezi ya kikosi cha wanandinga wa humu nchini ikiwa mara yake ya kwanza tangu atwae mikoba ya kuwanoa Harambee Stars.

Wachezaji wa kulipwa watajiunga na wenzao kambini kabla ya kikosi cha mwisho kutajwa kwa mechi za kundi F, kufuzu kwa kipute cha Kombe la Dunia mwaka ujao.

Kenya itamenyana na Gambia Alhamisi ijayo mjini Abidjan, Ivory Coast, katika mechi ya tano, kabla ya kuwaalika Gabon, tarehe 23 mwezi huu katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Harambee Stars inashikilia nafasi ya nne kundini kwa alama tano baada ya mechi nne.

Ivory Coast inaongoza kwa pointi 10, alama moja zaidi ya Gabon iliyo ya pili huku Burundi wakishikilia nafasi ya tatu kwa pointi saba.

Timu itakayomaliza ya kwanza katika kundi hilo wakati mechi hizo zitakapokamilika Septemba mwaka huu, itafuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *