Kampuni ya mafuta ya OLA Energy, inatarajiwa kutimua idadi ya wafanyakazi isiyojulikana katika mikakati ya kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi.
Taarifa ya kampuni hiyo imesema hali ngumu ya kiuchumi imeongeza gharama ya biashara na hawana budi kuratibu upya biashara zao kote nchini, na hali hiyo itasababisha kusimamishwa kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wake.
Kampuni hiyo pia imedokeza kuuza baadhi ya vituo vyake vya mafuta viungani mwa jiji la Nairobi.
Itakuwa mara ya pili kwa OLA Energy kuwafurusha wafanyakazi wake baada ya kuwalazimu maafisa wake 189 kustaafu mwaka 2019.
OLA Energy ina wafanyakazi zaidi ya 1,500 katika kaunti 17 nchini.