Kenya na Iran kuimarisha biashara ya mifugo na majani chai

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa kilimo na ustawi wa mifugo Mutahi Kagwe (Kushoto) na balozi wa Iran hapa nchini Ali Ghampour (Kulia).

Kenya inalenga kuimarisha biashara ya majani chai na mifugo baina yake na jamuhuri ya kiislamu ya Iran.

Waziri wa kilimo na ustawi wa mifugo Mutahi Kagwe, alisema taifa la Iran hutoa fursa nyingi za kibiashara licha vizingiti vilivyopo, akidokeza kuwa Iran ni soko kubwa la majani chai na mifugo kutoka Kenya.

Aliyasema hapo alipokuwa mwenyeji wa balozi wa Iran hapa nchini Ali Ghampour, kabla ya kuandaliwa kwa mkutano wa  pamoja wa ushirikiano kati ya Kenya na Iran mwezi Mei mwaka huu.

“Mazungumzo yetu yaliangazia kutatua changamoto katika uuzaji nje majani chai, pamoja na kutoa fursa ya ushirikiano kabla ya mkutao wa pamoja (JCC), utakaoandaliwa mwezi Mei mwaka 2025,” alisema waziri Kagwe.

Kulingana na mamlaka ya taifa kuhusu takwimu (KNBS), bidhaa zinazouzwa kutoka Kenya hadi nchini Iran, ziliongezeka hadi shilingi bilioni 6.7 kutoka shilingi bilioni 5.9 mwaka 2023.

Kwa upande mwingine, bidhaa zinazoagizwa kutoka Iran hadi hapa nchini ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 3.4 mwaka 2023, hadi shilingi bilioni nne mwaka jana.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *