Kenya na Azerbaijan zitaimarisha ushirikiano wa Kidiplomasia na wa kimaendeleo kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.
Haya yamesemwa na Rais William Ruto alipokutana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, katika uwanja wa Baku siku ya Jumapili .
Viongozi hao walijadiliana kwa kina kuhusu sekta za ushirikiano ikiwemo mafuta,gesi, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na matumizi ya kawi safi.
Ruto na mwenyeji wake walikutana pembezoni mwa kongamano la kimataifa la miji yaani World Urban Forum.
Aidha,mataifa hayo yalitathmini kuhusu pendekezo la Azerbaijan, kufungua kiwanda cha kusafisha mafuta eneo la Afrika Mashariki, na ushirikiano katika biashara na kutafuta soko la chai ya Kenya na bidhaa nyingine za kilimo nchini Azerbaijan