Polisi wanasa pombe haramu na mihadarati Nairobi na Pwani

Hii ni baada ya kufanywa kwa misako katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Nairobi katika juhudi za kuimarisha vita dhidi ya pombe haramu na mihadarati.

Dismas Otuke
1 Min Read

Polisi waliendesha misako na kunasa kiwango kikubwa cha pombe haramu na mihadarati katika maeneo ya Nairobi na Pwani. 

Washukiwa kadhaa waliokuwa wakiendesha biashara hiyo walikamatwa wakati wa misako hiyo.

Polisi walifanya misako katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Nairobi katika juhudi za kuimarisha vita dhidi ya pombe haramu na mihadarati.

Katika eneo la Jomvu, kaunti ya Mombasa, polisi wa kituo cha Mikindani walivamia mtaa wa Bangladesh na kuwakamata washukiwa waliokuwa na lita 120 za pombe haramu.

Aidha, polisi mjini Malindi, kaunti ya Kilifi waliendesha msako katika mtaa wa Kwa-Abudu na kuwatia mbaroni washukiwa wawili waliokuwa ma misokoto 140 ya bangi, ratili na karatasi za kupakia.

Katika kaunti ya Nairobi, polisi wa kituo cha Kahawa West walifanya msako mtaani Soweto na kuharibui lita 1,500 za pombe haramu aina ya kangara, lita 35 za chang’aa na mitungi ya kutengenezea pombe hiyo.

Share This Article