AUC yapongeza Kenya kuteuliwa kuandaa Mashindano ya Riadha Duniani 2029

Tume hiyo imeelezea matumaini ya Kenya kuandaa mashindano ya kufana na ya hadhi ya juu ikisema yatatoa fursa mwafaka kwa bara la Afrika kuonyesha umahiri wake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf, ameipongeza Kenya kwa kuteuliwa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029.

Youssouf amesema ni hatua kubwa kwa jiji la Nairobi kupata hadhi hiyo na jambo la kujivunia kwa Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika kupewa maandalizi ya mashindano hayo.

Aidha, alielezea matumaini yake ya Kenya kuandaa mashindano ya kufana na ya hadhi ya juu akisema yatatoa fursa mwafaka kwa bara  la Afrika kuonyesha umahiri wake nyumbani.

Jiji la Nairobi lilitangazwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029 mapema wiki hii, baada ya kushinda miji ya London – Uingereza na Roma – Italia.

Share This Article