Kesi kuhusu mauaji ya Sharon kuendelea leo Jumatano

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado.

Kesi kuhusu mauaji ya Sharon Otieno inayomkabili aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado, inatarajiwa kuendelea leo Jumatano, huku aliyekuwa msaidizi wake wa kibinafsi Michael Oyamo akitarajiwa kutoa ushahidi.

Hatua hii inajiri baada ya Jaji Cecilia Githua, kukataa ombi la Oyamo la kutaka kubadilisha mfumo wa ushahidi wake siku ya Jumatatu.

Jaji Githua alisisitiza kuwa ni hitaji la kisheria kwa mshtakiwa kuweka msingi wa kesi yake kabla ya mashahidi kutoa ushahidi wao.

Sharon Otieno aliuawa mwaka 2018 akiwa mja mzito, mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na Obado pamoja na washirika wake.

Washtakiwa katika mauaji hayo, wamekanusha kuyatekeleza.

Website |  + posts
Share This Article