Wanamichezo walioshinda na watakaoshinda medali za Olimpiki na katika mashindano ya Riadha Duniani, wanatarajiwa kuvuna pakubwa kutokana na kuanza kutekelezwa kwa mfumo mpya wa kuwatunuku na serikali.
Kulinagana na Katibu katika Wizara ya Michezo Elijah Mwangi, washindi wa dhahabu watapokea shilingi milioni 3 kutoka kiwango cha awali cha shilingi laki saba unusu huku washindi wa fedha wakitia kibindoni shilingi milioni 2 kutoka nusu milioni za awali.
Washindi wa medali za shaba watatuzwa shilingi milioni moja kutoka shilingi robo milioni za awali.
Hatua hii inalenga kuwamotisha wanamichezo wa Kenya wanaposhiriki mashindano ya kimataifa.
Mwangia alifuchua kuwa washindi wa medali za Kenya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita; wataitwa ili kupokea tuzo hizo