Rais wa Marekani Donald Trump amesema majeshi yake yanakaribia kumaliza vita nchini Iran, kufuatia mazungumzo ya moja kwa moja yanayoendelea kati ya mataifa hayo mawili.
Hata hivyo, kauli hiyo imekanushwa na aliyekuwa Balozi wa Iran, Abbas Khameyar aliyeitaja kuwa propaganda.
Khameyar amesisitiza kuwa ni sharti kuwe na ushirikishwaji wa jumuiya ya kimataifa kabla ya mwafaka wowote kusainiwa kati ya Marekani na Iran.
Marekani ikishirikiana na Israel imekuwa ikiendesha mashambulizi nchini Iran huku juhudi zote za mazungumzo ya kumaliza vita zikigonga mwamba.