Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (JKUAT) kimekanusha kuwa kamwe mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alikuwa mwanafunzi wake.
Kwenye barua iliyoandikwa Msajili wa Masuala ya Elimu chuoni humo Dkt. Aggrey Wanyama, Barasa hakufuzu kwa shahada ya ufundi wa mitambo ya umeme mwaka 2008 alivyodai na shahada aliyo nayo ni ghushi.
Awali, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi – EACC ilikuwa ikimchunguza mbunge huyo kwa madai ya kughushi cheti cha shahada.
Hatua hii ni pigo kubwa kwa Barasa ambaye amejitosa ulingoni kugombea kiti cha Ugavana wa kaunti ya Bungoma katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.