Museveni kuhutubia taifa Jumamosi

Kulingana na Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, PPU, hotuba hiyo itahusu masuala yenye umuhimu wa kitaifa.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kuhutubia wananchi wa taifa hilo Jumamosi Julai 4, 2026 saa 2 usiku, saa za Afrika Mashariki.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, PPU, hotuba hiyo itahusu masuala yenye umuhimu wa kitaifa.

Katika taarifa hiyo ya leo Jumatano, PPU ilisema kuwa hotuba hiyo ya Rais itarushwa mubashara kupitia vituo vyote vikuu vya redio na televisheni, pamoja na majukwaa ya mtandaoni kote nchini Uganda.

Kitengo cha Mawasiliano ya Rais kimewahimiza wananchi kufuatilia matangazo hayo na kusikiliza hotuba hiyo.

Taarifa hiyo haikutoa maelezo kuhusu masuala ambayo Rais Museveni anatarajiwa kuzungumzia, ikieleza tu kwamba hotuba hiyo itahusu masuala yenye umuhimu wa kitaifa.

Share This Article