Chui wa Congo kukabana na Three Lions ya Uingereza leo

Uingereza inayofunzwa na Thomas Tuchel iliongoza kundi L kwa alama 7, baada ya kuwashinda Croatia, na Panama, kabla ya kwenda sare na Ghana.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itashuka uwanjani Atlanta,Marekani kwa mechi ya raundi ya 32, huku wakilenga kuwa timu ya pili ya Afrika kufuzu kwa hatua ya 16 ya Kombe la Dunia.

The Leopards ya DRC wanaorejea Kombe la Dunia baada ya miaka 52,wanashikilia nafasi ya 46, huku Uingereza, wakikalia nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Dunia wa FIFA.

Itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana katika Kombe la Dunia na mara ya tatu kwa Uingereza, kuchuana na mpinzani wa Afrika katika hatua ya mwondoano.

Uingereza inayofunzwa na Thomas Tuchel iliongoza kundi L kwa alama 7, baada ya kuwashinda Croatia, na Panama, kabla ya kwenda sare na Ghana.

DRC yake  Sebastian Dessabre, ilimaliza miongoni mwa timu tatu bora  kutoka kundi K kwa pointi  4 ,wakishindwa na Colombia,  kutoka sare na Ureno na kuishinda Uzbekistan.

Mshindi wa mtanange wa leo  ambao utaanza saa moja usiku atachuana na Mexico katika awamu ya 16.

 

Share This Article