Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 haina budi kuwashinda mabingwa mara saba Nigeria kesho kutwa Mei 7,ili kuwa na fursa ya kujikatia tiketi kwa robo fainali ya kipute cha AFCON nchini Misri.
Kenya ilipoteza mechi ya pili kundini B jana jioni mabao 3-1, dhidi ya Tunisia, jana baada ya kupoteza mabao 3-2, kwa Morocco, kwenye mchuano wa ufunguzi,
Morocco wanaongoza kundi hilo kwa alama 4,sawia na Nigeria, baada ya timu hizo kutoka sare kappa jana huku Tunisia, ikiwa ya tatu kwa alama 3 nayo Kenya inashika mkia pasi na alama.
Katika mechi za leo jioni Ghan,a watapimana nguvu na majirani Senegal, katika derby ya Afrika magharibi kundini C huku Jamhuri ya Afrika ya kati ikitoana jasho na