Timu ya wanaume ya Kenya mita 100 kwa wanariadha wanne imeweka rekodi mpya ya kitaifa katika siku ya mwisho ya mbio za Dunia za kupokezana kijiti mjini Gaborone,Botswana.
Kikosi cha Kenya kilichowajumuisha Meshack Babu,Mark Odhiambo,Ronald Kiprono na bingwa wa Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala, kilimaliza katika nafasi ya tatu kwa sekunde 38.27.
Licha ya kuweka rekodi mpya ya kitaifa Kenya, ilikosa kufuzu kwa mashindano ya Dunia ya mwaka ujao jijini Beijing,Uchina.
Japan na Ghana ziliwahi tiketi ya moja kwa moja kwa mashindano ya Dunia, baada ya kutwaa nafasi za kwanza na pili mtawalia.
Kenya pia ilikosa kufuzu katika mbio za mita 400 kwa wanawake hali kadhalika mita 400 wanaume.