Nyumbani ni nyumbani! Aisha Jumwa arejea UDA

Jumwa alihama UDA mwishoni mwa mwezi Julai akidai kukosekana kwa demokrasia chamani kuwa sababu kuu ya kugura.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa zamani wa Jinsia Aisha Jumwa amerejea tena katika chama cha United Democratic Alliance (UDA), miezi mitatu tu baada ya kugura chama hicho tawala.

Jumwa alihama UDA mwishoni mwa mwezi Julai akidai kukosekana kwa demokrasia chamani kuwa sababu kuu ya kugura.

Awali, alitangaza nia ya kugombea Ugavana wa Kilifi.

Lakini baada ya kupokelewa rasmi UDA na Rais William Ruto siku ya Alhamisi katika Ikulu ya Mombasa, Jumwa aliahidi kutangaza mwelekeo wake hivi karibuni.

Kumekuwa na hekaheka katika chama cha UDA hususan miezi miwili iliyopita, ambapo ni maajuzi pia Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja alikitema na kuelekea ODM, akitumainia kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Kwa upande mwingine, mbunge wa Kasarani Ronald Karauri pia alitua UDA akilenga kutumia chama hicho kuwania ugavana wa Nairobi.

Share This Article